Isaiah 32:18-20

18 aWatu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani,
katika nyumba zilizo salama,
katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu.
19 bHata kama mvua ya mawe iangushe msitu
na mji ubomolewe kabisa,
20 ctazama jinsi utakavyobarikiwa,
ukipanda mbegu yako katika kila kijito,
na kuwaacha ngʼombe wako
na punda wajilishe kwa uhuru.
Copyright information for SwhNEN